ADVERTISE WITH US / TANGAZA NASI SASA
Advertise with us for three months,with an offer of free one month advertisement
contact email : adtillya@gmail.com
Monday, August 12, 2013
Chipukizi Aitoa kimasomaso Tanzania
Kijana Hamisi Mohamed ameipatia sifa Tanzania kwa kunyakua ubingwa wa dunia wa mchezo wa kuruka kamba uliofanyika Orlando nchini Marekani. Hamisi ambaye amelelewa katika kituo cha yatima cha dogodogo centre alipata nafasi ya kupongezwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu akiwa ameongozana pamoja na wachezaji wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya dunia. Tunampongeza sana Hamisi Mohammed kwa kuipeperusha vyema bendera ya tanzania.
na: Kilimanjaro Premium Lager
MSIMU WA KILI MUSIC TOUR HUU HAPA TENA
KILIMANJARO PREMIUM LAGER BONGE LA KIBURUDISHO KWA WATANZANIA LINAILETA ILE SAFARI YA WASHINDI NA ZIADA YA WASANII WA KTMA
TAMASHA HILI NI LAKO MWANANCHI "KIKWETU KWETU"
Waumini 44 wahofiwa kufariki Nigeria
kwa mujibu wa duru za Nigeria waumini zaidi ya 44 wamepigwa risasi na kufariki ndani ya msikiti wakati wakisali kaskazini mashariki mwa nigeria.
Mauaji hayo yametokea wakati waumini hao walipokuwa wanahudhuria swala ya asubuhi siku ya Jumapili, lakini taarifa ya tukio hilo ilipatikana jumatatu.
shambulio hilo limetokea katika mji wa Konduga katika jimbo la Borno, kilometa 35 kutoka mji mkubwa wa Maiduguri.
Bado hijafahamika wahusika wa shambulio hilo hasa japo kumekuwa na wasiwasi huenda kundi la Boko Haram limehusika. Kundi hilo limekuwa likitekeleza mauaji ya maelfu ya watu tangu mwaka 2009.
Taarifa ya. BBC
Barua ya wazi ya Mwinyi Kazimoto kwa TFF
AL MARKHIYA SPORTS CLUB
P O BOX 21923
DOHA, QATAR
TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
P O BOX 1574
DAR-ES-SALAAM
TANZANIA
YAH: KUOMBA MSAMAHA KWA CHAMA CHA MPIRA TANZANIA
Husika na kichwa cha habari hapo juu mimi mchezaji MWINYI KAZIMOTO naomba msamaha kwa kitendo nilichokifanya cha kuondoka kambini timu ya taifa na kuiacha nchi yangu katika kipindi kigumu hali ya kuwa walikuwa na mechi ngumu na muhimu dhidi ya Uganda.
Halikuwa lengo langu kuidhoofisha nchi yangu bali ni tamaa yangu ya kucheza mpira nje ya nchi ndiyo iliyonifanya niondoke katika kipindi hicho, na nashukuru mungu nimefanikiwa kupata team nchini Qatar, naamini watanzania wataipokea habari hii kwa vizuri.
Mwisho kabisa napenda kuwahakikishia watanzania na chama cha mpira kwa ujumla kwamba naahidi nitaitumikia nchi yangu muda wowote watakaponihitaji.
Natumai chama cha mpira na watanzania kwa ujumla watanielewa na watanisamehe.
Wenu mtiifu
MWINYI KAZIMOTO
Subscribe to:
Posts (Atom)