ADVERTISE WITH US / TANGAZA NASI SASA

Advertise with us for three months,with an offer of free one month advertisement

contact email : adtillya@gmail.com

Monday, October 21, 2013

POSA YA BOLINGO BY ALICIOS [OFFICIAL VIDEO]

Dk. Shein afungua semina ya mafunzo CCM makao makuu


Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amefungua semina ya mafunzo ya siku nne kwa Watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya nchini, leo katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo, Oktoba 21, 2013. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (zanzibar) Vuai Ali Vuai.

Picha ya: Mo Dewji blog

Afrika inajifunza nini toka China


Mpango wa kumwezesha kila mkulima aongeze mapato kwa mara mbili ifikapo mwaka 2020 nchini China. Kuanzisha soko la kuwasaidia wakulima wakodishe mashamba, kuwaruhusu wakulima kuendeleza uzalishaji wa kilimo kwa ukubwa wa kufaa kutahakikisha utimizaji wa mpango huo.

China haitekelezi utaratibu wa kubinafsisha ardhi. Watu wana haki ya kutumia ardhi badala ya kumiliki ardhi. Kwa mujibu wa utaratibu wa kutumia ardhi kwa mkataba kwa kila familia ya wakulima vijijini ulioanza kutekelezwa katika mwa miaka ya 70 ya karne iliyopita, wakulima wanaweza kutumia ardhi ndogondogo kwa muda mrefu baada ya kusaini mkataba. Kuanzishwa kwa utaratibu huo kuliwahamasisha wakulima wa China washughulikie uzalishaji, na kumetoa mchango mkubwa katika kuhakikisha uzalishaji wa kilimo na usalama wa vyakula, na kuongeza mapato ya wakulima. Lakini kutokana na kuinua kwa uwezo wa uzalishaji na kuenea kwa matumizi ya sayansi na teknolojia, vijiji vya China vinakabiliwa na tatizo la mashamba madogomadogo ambalo limepungua ufanisi wa matumizi ya ardhi.

Ofisa anayeshughulikia kazi ya kilimo wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Chen Xiwen alisema,

"Kwa mfano, kwa baadhi ya familia, watoto wao wameondoka na kwenda sehemu nyingine, wazee wanaobaki hawana uwezo wa kufanya kazi mashambani, au baadhi ya wakulima wanafanya kazi za vibarua mijini, hawataki kushughulikia uzalishaji wa kilimo tena. Kutokana na hali hizo, katika siku zilizopita China ilitunga sheria na sera ikiamua kuwa wakulima wanaweza kukodisha mashamba waliyokodishwa kwa mkataba."

Ingawa China imeamua kuwa wakulima wanaweza kukodisha mashamba kwa mkataba, lakini kutokana na ukosefu wa utaratibu na kanuni husika, uamuzi huo haufanyi kazi vijijini. Na mkutano mkuu wa 3 wa kamati kuu ya 17 ya chama cha kikomunisti cha China uliamua wazi kuwa wakulima wanaruhusiwa kupanga mpango wa matumizi ya ardhi kwa njia ya kuhamisha, uendeshaji, kukodisha na kushughulikia uzalishaji kwa ushirikiano wa kihisa, na kuendeleza uzalishaji wa kilimo kwa ukubwa wa kufaa. Mtafiti wa taasisi ya utafiti wa uchumi wa vijijini wa wizara ya kilimo ya China Bw. Zhao Yutian anaona kuwa hatua hiyo itasukuma mbele uchumi wa vijijini, akisema,

"Uamuzi huo utatoa mchango kwa pande mbili. Kwanza, uamuzi huo utatoa uungaji mkono wa kisera kwa kuanzisha utaratibu wa kupanga mpango wa matumzi ya ardhi; pili uamuzi huo utainua uwezo wa uzalishaji, kuongeza matumizi ya teknolojia, kuvutia mitaji ya nchini na nchi za nje, na kuhimiza mzunguko wa mazao ya kilimo. Uamuzi huo ni muhimu sana kwa maendeleo ya vijijini na kutatua masuala yanayohusu kilimo, vijiji na wakulima."

Kijiji cha Xiaogang cha wilaya ya Fengyang mkoani Anhui ni chimbuko la utaratibu wa kutumia ardhi kwa mkataba kwa kila familia ya wakulima vijijini nchini China. mwaka 1978, wakulima wa kijiji hicho walianza kusaini mkataba wa kulima mashamba kwa familia moja moja. Na hii ilikuwa mwanzo wa mageuzi ya utaratibu wa kukodi mashamba vijijini nchini China. Hivi sasa kijiji hicho kinakusanya mashamba madogo madogo tena kupanda zabibu na uyoga, kuendeleza uzalishaji wa kilimo kwa ukubwa, kilimo chenye sifa ya kipekee, na utalii wa vijijini. Kiongozi wa kijiji hicho Bw. Shen Hao alisema,

"Sisi sote tunaona kuwa, njia ya jadi ya uzalishaji kwa familia moja moja inaweza kuhakikisha maisha ya kimsingi ya wakulima, lakini haiwezi kuwasaidia wakulima wajitajirishe. Wakulima wanatakiwa washirikiane kuanzisha njia mpya ya uzalishaji, yaani kuwaruhusu wakulima kukodisha mashamba waliokodishwa kwa mkataba, kuendeleza uzalishaji wa kilimo kwa ukubwa unaofaa na kuendeleza kilimo cha kisasa, basi watatajirika."

Katika mji wa Daye ulioko mkoani Hubei ambao ni mkoa unaozalisha nafaka kwa wingi, mkulima Hou Anjie mwenye umri wa miaka 51 alikodi mashamba zaidi ya hekta 1300 kwa kusaini mikataba na wakulima elfu 20 kutoka vijiji vinane. Kwenye mashamba hayo kuna mpunga uliokomaa wenye rangi ya dhahabu, mashine za kilimo zinazofanya kazi na malori ya kubebea nafaka. Mwaka huu mashamba yake yamepata mavuno mazuri. Bw. Hou alisema,

"Tunalima mashamba na kuvuna mazao kwa mashine. Tunapanda, kuvuna na kuuza mazao na kununua mbolea kwa pamoja, bei za mazao na gharama ya uzalishaji ni chini zaidi kuliko wale wanaolima mashamba madogo madogo."

Bw. Hou Anjie alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, kabla ya uzalishaji mkubwa wa kilimo, wakulima walilima mashamba kwa familia moja moja, na mavuno ya nafaka yalikuwa kilo 4500 kwa hekta kwa mwaka. Hivi sasa akitumia teknolojia za kisasa na mashine, anapanda mazao kwenye mashamba hayo kwa pamoja, na mavuno ya nafaka yamefikia kilo 7500 kwa hekta. Hivyo wakulima wa huko wanapenda kukodisha mashamba yao. Bw. Hou alisema,

"Wakulima wanapenda kukodisha mashamba yao kwa sababu vijana wanafanya kazi za vibarua mijini, hivyo hakuna mtu anayeshughulikia uzalishaji mashambani, tena wakulima wakilima mashamba kwa familia moja moja, hawawezi kupata faida nyingi, kwa sababu bei za mbolea ya kemikali na dawa za kuulia wa dudu zote zimepanda."

Wengi kati ya wakulima zaidi ya milioni 700 wa China wanashughulikia uzalishaji wa kilimo kwenye mashamba madogo madogo, na ufanisi wa uzalishaji ni mdogo. Kuwaruhusu wakulima kukodisha mashamba waliokodishwa kwa mkataba, kutainua ufanisi wa uzalishaji wa kilimo, kuongeza mapato ya wakulima, na kuharakisha mchakato wa maendeleo ya miji nchini China.

Wataalamu walisema baada ya sera ya kuwaruhusu wakulima kukodisha mashamba kwa mkataba kutolewa, soko la kukodisha mashamba vijijini litaanzishwa haraka.

Makala ya Idhaa ya Kiswahili ya China : swahili.cri.cn

Huyu ndiye mtanzania aliyewahi kucheza na Theo Walcott


Anajulikana kama Edward Bahati Obara Odhiambo-Anaclet, amezaliwa tarehe 31 August 1985 (28)
mjini  Arusha, Tanzania ana kimo cha 5 futi na inch 9  (1.75 m) anayecheza nafasi ya mlizi (defender)
Timu alizocheza
anayoichezea sasa inaitwa club Brackley Town ya nchini uingereza
alianza kuichezea timu ya Oxford United wakati huo akiwa mwanafunzi kabla ya kujiunga na Southhampton kwa majaribio ambapo alicheza na Theo Walcott na Dexter Blackstock, hakufanikiwa kufuzu kucheza kikosi cha kwanza.
Maisha ya famili, anao ndugu wawili (kaka) Eric Odhiambo anayecheza mpira wa kulipwa katika klabu ya Bank Asya na Anaclet Odhiambo anayechezea timu ya Abingdon United.




Timu alizocheza awali akiwa U20 ni
2002–2003 Oxford United
2003–2004 Southampton



Timu alizocheza akiwa zaidi ya U20

2004–2006 Southampton (hakuwahi kufunga goli) 2004–2005 → Chester City (kwa mkopo) goli (0)
2005 → Yeovil Town (kwa mkopo) goli (0)
2005–2006 → Tamworth (kwa mkopo) mechi 8 goli (0)
2006–2008 Oxford United mechi 76 goli (4)
2008–2010 Stevenage Borough mechi 34 goli (3)
2010–2011 Newport County mechi 32 goli (0)
2011–2012 Gateshead mechi 25 goli (0)
2012– Brackley Town mechi 39 goli (1)



* Takwimu hizi zilinukuliwa tarehe 27 April 2013 (UTC)

Prof Jay kupanua soko la muziki wake


Mwanamuziki Joseph Haule au maarufu Prof Jay amekabidhiwa alama ya utambulisho wa bidhaa zake "Bar Code" za Muziki na shirika la GS1 Tanzania,

Prof Jay alinukuliwa akisema katika ukurasa wake wa facebook kwamba

"Leo nimekabidhiwa BARCODE yangu na shirika la GS1 TANZANIA , Hii itaniwezesha kuweza kutanua zaidi wigo wa soko la Muziki wangu na kuwafikia mashabiki wangu sehemu mbali mbali duniani na Quality ya juu zaidi, kwa wale wote waliokuwa wakiniulizia watapataje muziki wangu wa zamani na wa sasa tena kwa kiwango cha juu kabisa kaeni mkao wa kula....MUNGU AWABARIKI SANA!!"

Kila laheri Profesor Jay kuupeleka Muziki wa Tanzania anga za kimataifa kimasoko.

Zitto achukuliwe hatua chasema TUGHE


Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Ally Kiwenge alisema Dar es Salaam jana kwamba pamoja na hatua hiyo kukiuka sheria ya kazi na uhusiano kazini inayosema mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa, pia kitendo hicho si ajenda ya wafanyakazi hivi sasa.

Alisema ajenda ya wafanyakazi kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana kufa kupona katika kuhakikisha kuwa mshahara wa mfanyakazi unaongezeka kukidhi mahitaji ya mwezi mzima na kuwaondolea mzigo wa mikopo inayowaandama.

“Huu si wakati wa wafanyakazi kutaka kujua mishahara ya Rais au Waziri Mkuu, ajenda yetu kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi ili ukidhi mahitaji muhimu tofauti na sasa,” alisema Kiwenge.

Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) kimelaani hatua ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ya kutaja hadharani mshahara wa Rais na Waziri Mkuu na kuomba Spika Anne Makinda kuchukua hatua kwa vile ni ukiukaji wa sheria.

Chama hicho kimeeleza kusikitishwa na kitendo hicho kufanywa na Mbunge aliyehusika na upitishaji wa sheria hiyo huku wabunge wenyewe wakiwa wakali pale wananchi na wadau mbalimbali wanapohoji mapato yao.
Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Ally Kiwenge alisema Dar es Salaam jana kwamba pamoja na hatua hiyo kukiuka sheria ya kazi na uhusiano kazini inayosema mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa, pia kitendo hicho si ajenda ya wafanyakazi hivi sasa.

Alisema pamoja na hilo ni mkakati wa wafanyakazi sasa kuona wabunge wanatumia muda wao uliosalia kabla ya Bunge kuvunjwa kuhakikisha mambo makubwa mawili yanaingizwa katika Katiba mpya, moja ikiwa ni nafasi ya mfanyakazi kikatiba ikoje na pia kuona Katiba mpya inasema nini juu ya hatima ya maslahi ya wafanyakazi.

“Tunataka Katiba mpya itamke wazi juu ya mishahara ya wafanyakazi ili iwe ni ile inayokidhi haja,” alisema. Aeleza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wabunge wanaanza kutaja mishahara ya viongozi wa taifa hadharani kwa kudhani kuwa ndio njia sahihi ya kuwasaidia Watanzania bila kujua kuwa hatua hiyo itasababisha mgawanyiko wa matabaka na kuligawa Taifa, jambo ambalo ni la hatari.

“Sisi mishahara ya viongozi wote tunaifahamu na hata ya wabunge, lakini sheria inasemaje juu ya kutangaza mshahara wa mtu hadharani? Wafanyakazi wanaweza kuitaja lakini kwa vile wameandaliwa hawafanyi hivyo, wanazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.

“Naamini kama wafanyakazi wangekuwa ni watu wa kukusanyana na wangekuwa hawana maadili wangeweza kusema mengi ambayo yangeshangaza jamii lakini hawafanyi mambo kwa kukurupuka au kuutafuta umaarufu usio na msingi,” alisema.

Katibu Mkuu huyo wa Tughe alisema kwa kufuata mfano wa wafanyakazi, viongozi wakiwemo wabunge watoe kauli za kujenga nchi na si zenye kuashiria matabaka na ubaguzi, jambo linaloweza kusababisha migogoro mikubwa na kuliingiza taifa katika machafuko yasiyo na tija,” alisema.

Alisema wabunge wafahamu pia kwamba suala la mishahara litaendelea kubakia kuwa ni la mwajiri na mwajiriwa na ndio maana katika fomu au nyaraka nyingine zinazoelezea majukumu ya wabunge suala la mishahara na marupurupu yao haliwekwi wazi kwa vile ni siri kati yao na taasisi ya Bunge kisheria.

Mkuu wa mkoa akataa ombi la walevi Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi amekataa ombi la wakazi wa eneo la Chaduru katika Manispaa ya Dodoma kutaka kuwepo kwa Askari wa Usalama Barabarani kwa ajili ya kuvusha walevi ambao wamekuwa wakigongwa kwa wingi katika eneo hilo.

Dk Nchimbi alikataa ombi hilo juzi wakati alipotembelea na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo ikiwa siku ya kilele cha Siku ya Usalama Barabarani.

Aliwataka wananchi hao kuheshimu alama za Usalama Barabarani na hata kulinda alama hizo badala ya kuzitoa hali inayofanya magari kukosa ishara ya kutambua kama kuna alama au michoro katika eneo hilo. Wakati huo huo, jumla ya watu 727 wamepoteza maisha mkoani hapa kutokana na ajali za barabarani katika kipindi cha mwaka 2010 hadi Septemba mwaka huu.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Dodoma, Peter Sima alisema watu hao walipoteza maisha katika ajali 585 zilizotokea zikahusisha vifo hivyo katika maeneo mbalimbali mkoani Dodoma.

Alisema mbali na ajali hizo za barabarani pia jumla ya ajali 784 zilizotokea katika kipindi hicho zilisababisha watu 1919 kujeruhiwa. Pia alisema katika kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka huu ajali za barabarani 20 zilipungua kutoka ajali 313 kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka 2012 hadi ajali 293 katika kipindi cha Januari hadi Septemba 2013.

Alisema katika kipindi hicho pia ajali zilizohusisha pikipiki zilipungua na kutoka ajali 93 hadi ajali nane sawa na asilimia 8.6 kwa kipindi cha Januari hadi Septemba 2013.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2010 hadi Septemba mwaka huu vifo vilivyotokana na ajali za pikipiki vilikuwa 163 kati ya ajali 130 zilizohusisha vifo.

Alisema asilimia 78 ya ajali zinazotokea mkoani Dodoma zinasababishwa na makosa ya kibinadamu huku mwendo kasi na ulevi vikichangia kwa kiasi kikubwa.

Wednesday, September 18, 2013

Video Mpya TNG Squad - Crazy Man

Wilaya ya Chamwino Dodoma inakabiliwa na changamoto






Kuelekea siku ya Amani duniani Papa atoa wito





Kila mwaka ifikiapo tarehe 21 mwezi Septemba, Umoja wa Mataifa huadhimisha Siku ya Amani Duniani. Nayo kamati ya Kiekumeni ya Makanisa Duniani imewaomba waumini wote wa makanisa yake kuombea amani siku hiyo. 

Baba Mtakatifu baada ya katekesi yake siku ya jumatano kwa halaiki ya waumini na wahujaji waliokusanyika kwenye uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatikani, amewaalika waumini wakatoliki kote ulimwenguni kuungana na wakristo wenzao katika jitihada za kumwomba Mungu kuwajalia zawadi ya amani wote wenye kuishi kwenye maeneo yanayokumbwa na migogoro ya kivita.

Ni ombi la Baba Mtakatifu Francisko kwamba amani itawale kwenye mioyo ya watu wote, na kwamba kila mtu atajitahidi kuwashawishi viongozi wa dunia kutafuta suluhisho la kidiplomasia na kisiasa kwa ajili ya kuleta amani kwenye maeneo ambayo wakazi wake waanaendelea kuteseka kwa ajili ya migogoro.



Ni mazungumzo na majadiliano tu yanayoweza kuleta amani ya kudumu na kuhakikisha kwamba haki na heshima ya kila mwanadamu, na hasa wale walio dhaifu zaidi, inaendelezwa, asema baba Mtakatifu.                                                                                                                                                                              Chanzo: Radio Vatican Swahili








Chama tawala Rwanda chaongoza matokeo ubunge

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Bunge uliofanyika jana nchini Rwanda yanaonesha kuwa chama tawala cha RPF-Inkotanyi kinaelekea kupata ushindi mkubwa.

Matokeo ya awali yaliyotolewa usiku wa kuamkia leo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi yanaonesha kuwa chama cha RPF na washirika wake wamepata asilimia 76.07 ya asilimia 75 ya kura zote zilizopigwa hadi kufikia usiku wa kuamkia leo.

Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Rwanda Prof. Kalisa Mbanda amesema kuwa matokeo kamili ya awali ya uchaguzi wa jana wa Bunge yatatolewa leo mchana.

Chama cha Social Democratic Party (PSD) ni cha pili kwa kupata asilimia 13.01 ya kura kikifuatiwa na Liberal Party (PL) ambacho kimepata asilimia 9.38.

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa Bunge wa Rwanda yatatangazwa Septemba 25.

Friday, September 6, 2013

New Katy Perry - Roar (Official Video)

Siku chache kabla ya Mitihani Darasa la Saba Tutarajie nini?




Wakati akizindua mpango wa matokeo makubwa sasa waziri wa Elimu
alitaja malengo ya mpango huu kwa wizara yake yakianzia na matokeo
ya mitihani ya wanafunzi watakao fanya mtihani mwaka huu.

Chini ya mpango wa Matokeo Makubwa Sasa, Mawaziri na
Watendaji katika Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara yangu
tutapimwa utendaji wetu katika kufikia malengo yaliyopangwa katika
maabara ya elimu. Tutapimwa kwa vigezo vilivyo wazi.

Hali hiiitaimarisha usimamizi na utendaji kazi. Mimi Waziri na Kaimu
Katibu Mkuu wangu tumesaini mkataba na Mhe. Rais Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete kuwa tutatekeleza mikakati ya Matokeo Makubwa
Sasa na hatimaye kuinua kiwango cha ufaulu kwa elimu ya Msingi
na Sekondari kufika 80% ifikapo 2015. Kwa kuwa zoezi hili
litafanyika kwa uwazi, wananchi mtashuhudia matokeo ya upimaji
huo.

zaidi soma hapa:
Hotuba ya Waziri wa Elimu kuhusu BRN




Mamilionea 100 wanaweza kuzalishwa kila mwaka Tanzania


 
Mwenyekiti mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuwazawadia washindi wa mwezi augosti wa shindano aliloliasisi la kutwiti wazo bora la kuondoa umaskini nchini

Mratibu wa shindano hilo ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa taasisi ya uongozi na ujasiriamali (IMED), Dr Donath Olomi amesema jumla ya twiti 979 zilishindwanishwa na kumtaja mshindi wa kwanza, aliyejinyakulia zawadi ya shilingi milioni moja kuwa ni Bi Lilian Wilson ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha ardhi jijini Dar es salaam.

Aidha amemtaja mshindi wa pili aliyezawadiwa shilingi laki tano kuwa ni Bi Susana Senga ambaye ni Msanifu kurasa wa gazeti la Jamhuri, na nafasi ya tatu, iliyoambatana na zawadi ya shilingi laki tatu ilikwenda kwa Bw. Ombeni Kaaya mkazi wa Nzega anayefanya biashara ya mgahawa na saloon ya kike.


Chanzo: ITV News




Huu ndio wimbo mpya wa Shaggy


Njia Rahisi kwa Wasanii Wa Muziki Kujitangaza


Kupitia website ya Wabeeh wasanii wanaweza kuweka nyimbo zao na zikapata kununuliwa na kusikilizwa na mashabiki wao kote ulimwenguni zaid ingia hapa www.waabeh.com/market/music.html uchunguzi wa Blog hii umeng'amua kuwa karibu nusu ya wasanii wa muziki wa Kenya wanaitumia website hii kutengeneza pesa kwakua hili pia ni soko la muziki wao
wasanii wakubwa waliopo ni kama, Camp Mulla, Wyre, Jua Cali, Eric Wainaina, Kayamba Africa na wengineo

Album ya JUA CALI Yaiva


 


Ile Album kali ya Msanii mkongwe wa muziki wa Genge toka Kenya Jua Cali
inayotambulika kwa jina la Tugenge Yajayo imekemilika na inatarajiwa
kupatikana mitaani kuanzaia Septemba 12  Mwaka huu kwa mujibu wa Jua
album hiyo imesheheni nyimbo kali kama Baba Yao, Si Siri, Kuna Sheng na Jiachilie
aliyomshirikisha Jovial pia wadau wanaweza kuinunua online kupitia

Jua Cali's Album






Monday, September 2, 2013

Bomba la mafuta la Kenya-Uganda-Rwanda kuimarisha uchumi wa kanda

Kenya, Uganda na Rwanda zilikubaliana siku ya Jumanne (tarehe 25) juu ya ujenzi wa bomba ya mafuta itakayounganisha nchi hizi tatu katika juhudi ambazo viongozi wanasema zitaimarisha ushirikiano wa kanda na kupunguza gharama za nishati.


Hifadhi za mafuta zenye faida kibiashara zimegunduliwa huko Kenya na Uganda. Juu, Tullow Oil iko katika kisima cha Ngamia -1 katika Kaunti ya Turkana, Kenya. [Tullow Oil plc/AFP]


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Uganda Ugandan Yoweri Museveni walikutana nchini Uganda ambako walikubaliana kupanua ujenzi wao wa awali wa bomba ya mafuta ya Kenya-Uganda hadi Ruanda.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa alisoma taarifa ya pamoja kutoka kwa marais baada ya mkutano wa pande tatu, na kusema kuwa nchi tatu hizo pia zilikubaliana kufanya kazi kwa ajili ya bomba la pili.

"Bomba ya kwanza ni upanuaji wa hii ya sasa ambayo inaleta bidhaa za mafuta kutoka Mombasa hadi Eldoret Kenya hadi Kampala (Uganda) na Kigali (Rwanda)," Kutesa aliwaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya Rais wa Uganda siku ya Jumatano. "Bomba itatengenezwa pia kuwa na mfumo wa kurejesha ili wakati tunapokuwa na bidhaa zetu wenyewe zilizotengenezwa iweze kusukuma bidhaa hizo kurudi nyuma."

Bomba la pili litajengwa ili kuchukua mafuta ghafi kutoka Kampala hadi Lamu, Kutesa alisema.

Makubaliano hayo hayakutoa ratiba wala gharama za ujenzi, hata hivyo, mradi wa bomba la Kenya-Uganda utagharimu shilingi za Kenya biloni 26 (dola milioni 302).

Kenya na Uganda zimekuwa kwa pamoja zikitafuta mkandarasi wa kujenga bomba la kilomita 320, kwa mujibu wa Katibu Mkuu anayeondoka madarakani wa Wizara ya Nishati, Patrick Nyoike. Nchi mbili hizo zilikuwa zinatafuta mkandarasi mpya baada ya kumalizwa kwa mkataba wa kampuni ya Tamoil East Africa Limited mwezi Septemba mwaka 2012 kutokana na kuchelewa, alisema.

Makubaliano haya yanakuja wakati muhimu ambapo Uganda na Kenya zimegundua hifadhi za mafuta za kuaminika kibiashara, alisema, na kwamba mradi huo utasaidia kuimarisha mahusiano ya kiuchumi baina ya nchi jirani.

"Bomba litaondosha usafirishaji wa sasa wa magari ya mafuta na matokeo yake kupunguza bei ya mafuta kwa watumiaji," aliiambia Sabahi.

Mbali ya kuimarisha muda wa usafiri, bomba pia litapunguza ajali za barabarani za mara kwa mara zinazohusisha magari ya mafuta yanayovuka mipaka, alisema Katibu wa Baraza kwa Masuala ya Afrika Mashariki, Phyllis Kandie.

Kwa sasa, nchi hizo mbili zinaagiza bidhaa za mafuta kutoa eneo la Ghuba kupitia Bahari ya Hindi hadi bandari ya Mombasa ambako kuna vinu vya kusafisha mafuta.

Kandie alisema kwamba bomba sio tu zitaifaidi Kenya, Uganda na Ruanda, bali pia Tanzania na Burundi. Gharama iliyopungua ya kusafirisha mafuta pia itapunguza gharama za bidhaa na kuimarisha hali za maisha za watu wa kanda hii, aliiambia Sabahi.

Mradi wa bomba ni mmoja kati ya mingi iliyofikiwa na Kenya, Uganda na Rwanda. Nchi hizo pia zilikubaliana kuharakisha utelekezaji wa kadi za utambulisho za elektroniki na visa za utalii kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, kuwezesha uzalishaji wa umeme, kufufua mitandao ya reli na kujenga njia ya reli ya kiwango baina ya Kenya na Uganda ambayo itapanulia hadi Rwanda.

Kenya itasimamia masuala ya uzalishaji umeme na usambazaji wake pamoja na maendeleo ya bomba la mafuta. Uganda itasimamia masuala ya maendeleo ya reli na shirikisho la kisiasa, na Rwanda itakuwa na jukumu la kutoa ushuru, viza moja ya utalii, na kitambulisho cha kielektroniki kwa EAC.

Licha ya ahadi, madereva wa magari ya mafuta wa Kenya walizipokea habari za ujenzi wa bomba kwa hisia mchanganyiko.

Johnstone Njoroge, mwendesha gari la mafuta wa Kenya mwenye umri wa miaka 45, ambaye anasafirisha mafuta kutoka bandari ya Mombasa hadi Uganda na Rwanda, alisema kuwa bomba zinatishia upatikanaji riziki kwa familia nyingi zinazotegemea usafirishaji huo.

"Nimekuwemo katika sekta ya usafirishaji kwa miaka saba," alisema. "Miezi kumi iliyopita, nikamudu kununua gari langu mwenyewe la mafuta ambalo ninalitumia kwa kusafirishia mafuta."

"Bomba la mafuta la Kenya-Uganda-Rwanda sio zuri kwangu kwa sababu ikiwa ikiharakishwa na kumaliza chini ya miaka miwili, sitakuwa nimerejesha pesa ambazo nilinunulia gari," alisema.

Mohammed Hussein Abdille, mwenye umri wa miaka 36 na mmiliki wa gari la mafuta, alisema kuwa bomba haitaathiri biashara yake.

Bomba zitatoa njia tu kwa usafirisishaji wa masafa marefu, lakini fursa za kusafirisha bidhaa zitokanazo na mafuta, aliiambia Sabahi.

"Serikali zinapaswa kufuatilia kwa haraka ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sababu ingewaruhusu wasafirishaji kuwa huru kufanya biashara katika nchi yoyote," alisema

Chanzo: www.sabahionline.com

Kijukuu YOUNG DEE New Tanzanian music 2013

Diamond Platnumz - Number One Official Music Video HD 2013