Kenya, Uganda na Rwanda zilikubaliana siku ya Jumanne (tarehe 25) juu ya ujenzi wa bomba ya mafuta itakayounganisha nchi hizi tatu katika juhudi ambazo viongozi wanasema zitaimarisha ushirikiano wa kanda na kupunguza gharama za nishati.
Hifadhi za mafuta zenye faida kibiashara zimegunduliwa huko Kenya na Uganda. Juu, Tullow Oil iko katika kisima cha Ngamia -1 katika Kaunti ya Turkana, Kenya. [Tullow Oil plc/AFP]
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Uganda Ugandan Yoweri Museveni walikutana nchini Uganda ambako walikubaliana kupanua ujenzi wao wa awali wa bomba ya mafuta ya Kenya-Uganda hadi Ruanda.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa alisoma taarifa ya pamoja kutoka kwa marais baada ya mkutano wa pande tatu, na kusema kuwa nchi tatu hizo pia zilikubaliana kufanya kazi kwa ajili ya bomba la pili.
"Bomba ya kwanza ni upanuaji wa hii ya sasa ambayo inaleta bidhaa za mafuta kutoka Mombasa hadi Eldoret Kenya hadi Kampala (Uganda) na Kigali (Rwanda)," Kutesa aliwaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya Rais wa Uganda siku ya Jumatano. "Bomba itatengenezwa pia kuwa na mfumo wa kurejesha ili wakati tunapokuwa na bidhaa zetu wenyewe zilizotengenezwa iweze kusukuma bidhaa hizo kurudi nyuma."
Bomba la pili litajengwa ili kuchukua mafuta ghafi kutoka Kampala hadi Lamu, Kutesa alisema.
Makubaliano hayo hayakutoa ratiba wala gharama za ujenzi, hata hivyo, mradi wa bomba la Kenya-Uganda utagharimu shilingi za Kenya biloni 26 (dola milioni 302).
Kenya na Uganda zimekuwa kwa pamoja zikitafuta mkandarasi wa kujenga bomba la kilomita 320, kwa mujibu wa Katibu Mkuu anayeondoka madarakani wa Wizara ya Nishati, Patrick Nyoike. Nchi mbili hizo zilikuwa zinatafuta mkandarasi mpya baada ya kumalizwa kwa mkataba wa kampuni ya Tamoil East Africa Limited mwezi Septemba mwaka 2012 kutokana na kuchelewa, alisema.
Makubaliano haya yanakuja wakati muhimu ambapo Uganda na Kenya zimegundua hifadhi za mafuta za kuaminika kibiashara, alisema, na kwamba mradi huo utasaidia kuimarisha mahusiano ya kiuchumi baina ya nchi jirani.
"Bomba litaondosha usafirishaji wa sasa wa magari ya mafuta na matokeo yake kupunguza bei ya mafuta kwa watumiaji," aliiambia Sabahi.
Mbali ya kuimarisha muda wa usafiri, bomba pia litapunguza ajali za barabarani za mara kwa mara zinazohusisha magari ya mafuta yanayovuka mipaka, alisema Katibu wa Baraza kwa Masuala ya Afrika Mashariki, Phyllis Kandie.
Kwa sasa, nchi hizo mbili zinaagiza bidhaa za mafuta kutoa eneo la Ghuba kupitia Bahari ya Hindi hadi bandari ya Mombasa ambako kuna vinu vya kusafisha mafuta.
Kandie alisema kwamba bomba sio tu zitaifaidi Kenya, Uganda na Ruanda, bali pia Tanzania na Burundi. Gharama iliyopungua ya kusafirisha mafuta pia itapunguza gharama za bidhaa na kuimarisha hali za maisha za watu wa kanda hii, aliiambia Sabahi.
Mradi wa bomba ni mmoja kati ya mingi iliyofikiwa na Kenya, Uganda na Rwanda. Nchi hizo pia zilikubaliana kuharakisha utelekezaji wa kadi za utambulisho za elektroniki na visa za utalii kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, kuwezesha uzalishaji wa umeme, kufufua mitandao ya reli na kujenga njia ya reli ya kiwango baina ya Kenya na Uganda ambayo itapanulia hadi Rwanda.
Kenya itasimamia masuala ya uzalishaji umeme na usambazaji wake pamoja na maendeleo ya bomba la mafuta. Uganda itasimamia masuala ya maendeleo ya reli na shirikisho la kisiasa, na Rwanda itakuwa na jukumu la kutoa ushuru, viza moja ya utalii, na kitambulisho cha kielektroniki kwa EAC.
Licha ya ahadi, madereva wa magari ya mafuta wa Kenya walizipokea habari za ujenzi wa bomba kwa hisia mchanganyiko.
Johnstone Njoroge, mwendesha gari la mafuta wa Kenya mwenye umri wa miaka 45, ambaye anasafirisha mafuta kutoka bandari ya Mombasa hadi Uganda na Rwanda, alisema kuwa bomba zinatishia upatikanaji riziki kwa familia nyingi zinazotegemea usafirishaji huo.
"Nimekuwemo katika sekta ya usafirishaji kwa miaka saba," alisema. "Miezi kumi iliyopita, nikamudu kununua gari langu mwenyewe la mafuta ambalo ninalitumia kwa kusafirishia mafuta."
"Bomba la mafuta la Kenya-Uganda-Rwanda sio zuri kwangu kwa sababu ikiwa ikiharakishwa na kumaliza chini ya miaka miwili, sitakuwa nimerejesha pesa ambazo nilinunulia gari," alisema.
Mohammed Hussein Abdille, mwenye umri wa miaka 36 na mmiliki wa gari la mafuta, alisema kuwa bomba haitaathiri biashara yake.
Bomba zitatoa njia tu kwa usafirisishaji wa masafa marefu, lakini fursa za kusafirisha bidhaa zitokanazo na mafuta, aliiambia Sabahi.
"Serikali zinapaswa kufuatilia kwa haraka ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sababu ingewaruhusu wasafirishaji kuwa huru kufanya biashara katika nchi yoyote," alisema
Chanzo: www.sabahionline.com