ADVERTISE WITH US / TANGAZA NASI SASA

Advertise with us for three months,with an offer of free one month advertisement

contact email : adtillya@gmail.com

Monday, August 12, 2013

JE UNATAFUTA AJIRA? TEMBELEA TOVUTI HII

ajirazetu.com

Kanuni za Bunge (Soma hapa)

www.parliament.go.tz/docs/kanuni07/mbili.pdf

Chipukizi Aitoa kimasomaso Tanzania


Kijana Hamisi Mohamed ameipatia sifa Tanzania kwa kunyakua ubingwa wa dunia wa mchezo wa kuruka kamba uliofanyika Orlando nchini Marekani. Hamisi ambaye amelelewa katika kituo cha yatima cha dogodogo centre alipata nafasi ya kupongezwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu akiwa ameongozana pamoja na wachezaji wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya dunia. Tunampongeza sana Hamisi Mohammed kwa kuipeperusha vyema bendera ya tanzania.

na: Kilimanjaro Premium Lager

MSIMU WA KILI MUSIC TOUR HUU HAPA TENA

KILIMANJARO PREMIUM LAGER BONGE LA KIBURUDISHO KWA WATANZANIA LINAILETA ILE SAFARI YA WASHINDI NA ZIADA YA WASANII WA KTMA


TAMASHA HILI NI LAKO MWANANCHI "KIKWETU KWETU"

Waumini 44 wahofiwa kufariki Nigeria


kwa mujibu wa duru za Nigeria waumini zaidi ya 44 wamepigwa risasi na kufariki ndani ya msikiti wakati wakisali kaskazini mashariki mwa nigeria.

Mauaji hayo yametokea wakati waumini hao walipokuwa wanahudhuria swala ya asubuhi siku ya Jumapili, lakini taarifa ya tukio hilo ilipatikana jumatatu.

shambulio hilo limetokea katika mji wa Konduga katika jimbo la Borno, kilometa 35 kutoka mji mkubwa wa Maiduguri.

Bado hijafahamika wahusika wa shambulio hilo hasa japo kumekuwa na wasiwasi huenda kundi la Boko Haram limehusika. Kundi hilo limekuwa likitekeleza mauaji ya maelfu ya watu tangu mwaka 2009.

Taarifa ya. BBC

Barua ya wazi ya Mwinyi Kazimoto kwa TFF




AL MARKHIYA SPORTS CLUB
P O BOX 21923
DOHA, QATAR
TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
P O BOX 1574
DAR-ES-SALAAM
TANZANIA

YAH: KUOMBA MSAMAHA KWA CHAMA CHA MPIRA TANZANIA
Husika na kichwa cha habari hapo juu mimi mchezaji MWINYI KAZIMOTO naomba msamaha kwa kitendo nilichokifanya cha kuondoka kambini timu ya taifa na kuiacha nchi yangu katika kipindi kigumu hali ya kuwa walikuwa na mechi ngumu na muhimu dhidi ya Uganda.
Halikuwa lengo langu kuidhoofisha nchi yangu bali ni tamaa yangu ya kucheza mpira nje ya nchi ndiyo iliyonifanya niondoke katika kipindi hicho, na nashukuru mungu nimefanikiwa kupata team nchini Qatar, naamini watanzania wataipokea habari hii kwa vizuri.
Mwisho kabisa napenda kuwahakikishia watanzania na chama cha mpira kwa ujumla kwamba naahidi nitaitumikia nchi yangu muda wowote watakaponihitaji.
Natumai chama cha mpira na watanzania kwa ujumla watanielewa na watanisamehe.
Wenu mtiifu

MWINYI KAZIMOTO

Tuesday, July 9, 2013

Serekali ya Kenya yabadili wazo la Laptop kwa wanafunzi


Amekaririwa katibu mkuu wa wizara ya elimu nchini Kenya Prof Jacob Kaimenyi akitoa kauli kwamba kutokana na hofu iliyopo kwamba TEKNOHAMA ina badilika katika kipindi kifupi sana, na kwa miaka mitano ijayo kompyuta watakazo kuwa wanatumia wanafunzi hao zitakuwa zimepitwa na wakati, hivyo wameamua kutotekeleza mradi huo ili kuepuka nchi kuwa dampo la bidhaa zilizopitwa na wakati, pia wameona kuwa watoto wanapendelea kompyuta za mguso (touch screen) kuliko zitumiazo kipanya (mouse), imeeleza taarifa hiyo.

Zaidi: www.standardmedia.co.ke/?articleID=2000087958&story_title=government-considering-tablets-over-laptops

Huyu ndiye mpinzani wa Czeck Chelsea


Golkipa wa zamani wa Fulham Mark Schwarzer mwenye umri wa miaka 40 amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Chelsea ya England, goli kipa huyo aliwahi kuzichezea timu za Bradford City na Middlesbrough kabla ya kujiunga na Fulham mwaka 2008.

Chanzo: BBC Sport

Mashindano ya EURO kwa wanawake kufanyika Sweden

Mashindano ya soka ama mpira wa miguu kwa wanawake yanatarajiwa kuanza hapo July 10 hadi 28, timu zimepangwa katika makundi matatu ya timu nne nne, tayari vigogo wa soka hilo Ufaransa na Wingereza pamoja na wenyeji Swedeni wameonesha nia yakulinyakua kombe hilo, timu mbili za kwanza katika kila kundi zitakutana kwaajili ya robo fainali, michezo hiyo itapigwa katika miji mbalimbali yanayo uzunguka mji wa Stockholm katika hatua ya makundi ambayo ni Gothenburg, Halmstad, Vaxjo, Kalmar, Norrkoping and Linkoping  na fainali katika mji wa Solna, pembezoni mwa Stockholm.

Zaidi: www.bbc.co.uk/sport/0/football/23022779

Sikiliza wimbo mpya MKOLONI ~ BILA SABABU

 

Epiq Bongo Star Search Yaendelea na Usaili

Baadhi ya Washiriki Mjini Zanzibar walipokuwa wakijiandaa kuingia katika usaili katika hoteli ya Bwawani

Washindi wanne wamepatikana Zanzibar kwenye usaili wa Epiq Bongo Star Search uliofanyika wikiendi hii katika ukumbi wa Bwawani, usaili huo utaendelea tena jijini Mbeya katika ukumbi wa Club Vybes kuanzia Jumatano tarehe 10 na kumalizika Alhamisi tarehe 11 July.

Habari na  Picha kwa hisani ya:  Epiq BSS



Saturday, July 6, 2013

TID EXCLUSIVE INTERVIEW WITH SPORAH..!

ndege ya Boeing 777 yaanguka huko San Francisco airport

ndege ya Boeing 777 imeanguka katika uwanja wa ndege wa San Fransisco karibu na mji wa kibiashara wa North California Marekani

maelezo zaidi bbc.co.uk yanasema:

Pictures posted on Twitter showed passengers jumping down the inflatable emergency slides and leaving the area, as plumes of smoke rise from the plane.

Fire fighters and rescue teams are at the scene of the downed Asiana Airlines Flight 214, which had taken off from South Korea's capital, Seoul.
The cause of the crash is unclear. Early indications suggest the plane came in too short and hit the seawall at the airport.

zaidi nenda www.bbc.co.uk/news/world-us-canada-23214513

Download Joh Makini ft FundiSamweli-Nikumbatie

Baada ya mapacha wa 3 sasa ni Ndege wa 3


wasanii watatu wa kike wa Bongo wameungana na kuunda kundi lao linalijulikana kwa jina la Ndege watatu, wasanii hao ni Puline Zongo, Joan Matovolwa na Khadija Mnoga "Kimobiteli" ambao wamesharekodi wimbo mmoja hadi sasa, kila laheri Ndege watatu na ujio wenu huo

                                         Picha na Dewji blog

Mpango wa maendeleo wa Taifa usome hapa

ku download mpango fuata hapa:   www.tanzania.go.tz/pdf/MPANGO%20WA%20MAENDELEO%20DGTO%20MPYA.pdf

Ofisi ya Rais Tume ya Mipango

Mapinduzi ya Kijeshi Misri


 baada ya mvutano mkali katika mji wa Cairo nchini Misri huyu ndiye aliyeteuliwa na jeshi kuwa Rais wa mpito baada ya mapinduzi ya kijeshi ya kumwondoa madarakani Rais Mohamed Morsi, na huyu ndiye Rais mpya anayejulikana kama Adly Mansour aliyekuwa Jaji mkuu nchini humo

hawa walikuwa ni wafuasi wa Rais aliyepinduliwa Mohamed Morsi wakipinga kitendo cha Jeshi lao kumpindua mtu waliyekuwa wakimuamini


Paulsen bado nina mwamini Kaseja


Licha ya timu ya Simba kujifaragua kuwa hawatomsajili Juma K Juma, kocha wa Taifa Stars Kim Paulsen amesema bado anamwamini nahodha huyo wa timu yake na kwamba bado ataendelea kuwa mchezaji chaguo la kwanza kwa magolikipa wa Stars, Paulsen alitangaza kikosi cha CHAN kitakacho ivaa Uganda mapema mwezi huu

Mechi ya Stars Cranes yapata waamuzi

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) itakayofanyika Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi hao ni Thierry Nkurunziza atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake watakuwa Jean Claude Birumushahu na Pascal Ndimunzigo. Mwamuzi wa akiba (fourth official) ni pacifique Ndabihawenimana.

Kamishna wa mechi hiyo Gebreyesus Tesfaye kutoka Eritrea. Tesfaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Eritrea na mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya CHAN.
                                                 
                                                Taarifa na : TFF website

Maeneo ya kujidai mjini Dodoma

hii ni picha ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unaweza kutembelea hapa na kujionea shughuli mbalimbali za Bunge na Ofisi ya Bunge wakati wowote, Bunge letu lipo katika jengo hili la kisasa kabisa

hapa panaitwa Nyerere Square, mahali ulipo mnara wa kumbukumbu wa Baba wa Taifa Mwl J.K Nyerere, unaweza kutembelea na kukaa au kupiga picha pia ipo migahawa ya kawaida kwa chakula na vinywaji

hili ni kanisa lililopo mjini kati na linafahamika kama kanisa la Cathedral, unaweza kutembelea na kupiga picha za kumbukumbu hapahapa mjini dodoma